SHARE:
Niliamua kuandaa makala yangu ili iwe mfano kwa kuwa kumekuwa na dhana potofu ya kwamba Wanawake wamekuwa nyuma sana katika nyanja mbalimbali na kupitia maisha ya Miriam Makeba kwangu nilihisi alikuwa mfano bora sit u kwa akina Mama tu bali jamii nzima ya Waafrika.
Miriam Makeba kupitia kipaji chake cha muziki aliweza kushiriki katika harakati za kuwaletea watu wa Afrika ya Kusini uhuru wa kweli kutoka katika utawala wa kibaguzi wa Weupe wachache kiasi kwamba kwa kutambua nguvu ya muziki wake watalwala wale walimchukia sana Miriam Makeba na wakamchukulia kuwa ni mtu â € œhatariâ € sana kwao
Tumejifunza kuwa muziki ni dawa,muziki ni ajira pia kama makala hiyo tunaona Miriam Makeba aliuchukulia muziki wake kama sehemu ya maisha yake na kwa kutambua nguvu ya muziki wake akaweza kuwaunganisha si tu ndugu zake wa Afrika ya Kusini bali Bara zima la Afrika na Duniani kwa ujumla.
Maisha yake yalikuwa ya misukosuko sana hata hivyo licha ya kadhia aliyokuwa akikumbana nayo kutoka Serikalini na pia katika maisha yake ya kawaida, Miriam aliwahi kuachwa na aliyewahi kuwa mumewe wa kwanza tena akiwa na maumivu makali kitandani kwa ugonjwa wa kansa ya matiti lakini aliweza kuyabeba maumivu yale na kamwe hakukata tamaa!
Wanawake wengi wamekuwa wakikata tama mapema katika shughuli mbalimbali lakini niliamini maisha ya Miriam Makeba yalipaswa kuwa mfano kwa akina Mama wengi zaidi hapa nyumbani Tanzania na zaidi katika siku yao (Womanâ € ™s day) na pengine kipindi/makala yangu ingeleta mwanga mpya kwa akina Mama na ndiyo maana hata Mtangazaji/Msimulizi niliamua kumuweka wa Kike ili kuleta upekee katika makala yangu
Binafsi naamini Wanawake wanaweza tena kwa kiwango kikubwa pengine hata zaidi ya Wanaume!
Download : 18872_mainapplicationmediaradioemmanuelmsigwa.doc
📝Read the emotional article by @nokwe_mnomiya, with a personal plea: 🇿🇦Breaking the cycle of violence!https://t.co/6kPcu2Whwm pic.twitter.com/d60tsBqJwx
— Gender Links (@GenderLinks) December 17, 2024
Comment on Radio Documentary