Experience in the field of health nurses_ Homa ya Jiji_ 14 June 2016


Date: June 14, 2016
  • SHARE:

Name of the story:  Experience in the field of health nurses

Name of the media house: Homa ya Jiji

Country: Tanzania

Synopsis

Brief description of the item of work you submitted and motivation of why it is a good example of gender awareness and sensitivity in advancing gender equality Post-2015.

Baada ya kufika katika moja ya zahanati katika Kata ya Igale ambayo ipo Katika Kijiji cha Izumbwe ambayo iliteketea kwa moto ndipo nilipoona nianze kuulizia hali ya huduma ya Afya katika Kata nzima ipoje.

Kwa ujumla hali ni mbaya na hauwezi kuamini lakini wahenga wamesema tembea uone nami nimeyaona baada ya kutembelea katika Kata ya Igale na kujionea katika Nyanja ya Afya wauguzi wakitumia tochi za simu kuzalisha katika chumba maalum cha uzazi(Labour) ni katika zahanati zote zilizopo katika Kata hiyo.

Huduma za Afya hazipatikani baada ya saa 9 mchana hadi kesho yake ndipo zitapatikana na kama mtu akizidiwa ama akitokea Mama Mja mzito anayetaka kujifunguwa ni shauri yake,hayo yote yapo Kata ya Igale.

Kata ya Igale iliyokaa kijiografia katika milima na mabonde ina idadi ya Zahanati tatu zisizokuwa na maji safi na salama,umeme hata wa nguvu ya jua hakuna,nyumba za watumishi hakuna lakini kibaya zaidi Kata hiyo ina idadi ya Vijiji vitano vilivyopakana kwa umbali mrefu kutoka Kijiji kimoja kwenda kingine lakini Zahanati ndiyo hizo na hakuna matumaini ya kujengwa kwa kituo cha Afya hivi karibuni.

Nimeona Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya haijatimiza wajibu wake katika Zahanati ya Holongo Zahanati iliyojengwa kwa nguvu za wananchi kwa takribani miaka 10 hadi mtamba wa panya ambapo kwa mujibu wa Sera ya Afya hatua ya upauaji na kukamilisha ujenzi huo(finishing) ni jukumu la Serikali lakini haijafanya hivyo.

Lugha chafu za wauguzi wakiwakaripia wagonjwa kuwa wananuka uchafu wakaoge kwanza na ndipo warejee kutibiwa. lakini pia wanafanyakazi wanadaiwa kuwatoza akina mama wajawazito wanaojifungulia nyumbani wanapewa adhabu ya faini kati ya Sh.5,000 hadi 20,000 zisizo na stakabadhi hata kama umezalia njiani ukielekea katika Zahanati.

Kuna kila sababu ya kuwasaidia wananchi wa Kata ya Igale,Halmashauriya Wilaya ina jukumu kubwa la kuwasaidia wanawake na watoto wa Igale na maeneo mengine wakiwemo wadau mbalimbali wa sekta ya Afya.

Background

Why did you produce the story? What problem or context is it responding to?

Nimekutana na changamoto nyingi katika kufuatilia habari hii ambayo ni ya kiuchunguzi kutokana na ghala nilizozitumia kubwa kwa ajili ya usafiri kutembelea Vijiji vitano ambavyo ni Shongo,Igale,Horongo,Izumbwe na Itaga ambavyo vimekaa mbali katika milima na mabonde na misitu ambapo ilikuwa ni hatari pia kwangu kutokana na watendaji,wauguzi na waganga wa zahanati kuonekana wakichukia kuhojiwa na hasa yale maswali yaliyokuwa yakiwagusa moja kwa moja na hivyo kujenga mazingira ya hatari kwa usalama na hivyo nilikuwa nikilazimika kutokula vyakula ovyo,kutotumia njia moja na muda fulani nilikuwa nikifika kijijini bila kutoa taarifa wala miadi kwa watu niliokuwa nikipaswa kuwahoji na matokeo yake nilikuwa nikiwakosa na hivyo kuvuta muda mrefu wa kuikamilisha habari ya Afya ambapo nimetumia takribani miezi miwili.

Imeshatokea kukosa ushirikiano kwa baadhi ya wanakijiji wakihofia kuadhibiwa na watendaji wa Kijiji huku wengine wakidai kuwa wanahofia kuchomwa sindano za sumu watakapougua endapo watabainika kuwa wamenipa ushirikiano wa kunielezea hali halisi ya huduma ya Afya.

Usafiri mkubwa niliokuwa nikiutumia ulikuwa ni pikipiki almaarufu Boda boda ambazo kutokana na barabara mbovu nilijikuta nikiugua mgongo na kiuno kwa muda wa mwezi mmoja nikiwa ninapumzika nyumbani na kwa mujibu wa maelezo ya Dkt.nilishauriwa kutofanya kazi ngumu na kutakiwa kupumzika muda mrefu kuliko kutembea.

Key objectives

What did you hope to achieve with this coverage?

Matokeo yameanza kujitokeza tangu nimeandika hii habari ambapo tayari Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya imefika kutoka semina kwa wauguzi na waganga wa zahanati zote za Kata ya Igale kuwakumbusha maadili yao ya kazi,kutumia lugha ya upole na unyenyekevu.

Ninashukuru pia katika safari hiyo Ofisi ya Mkurugenzi ilinialika nami niliungana nao na kushuhudia zoezi hilo likifanyika na hatimaye kufanikiwa kuwahoji baadhi ya wahudumu wa afya ambao walipata semina hiyo hali iliyonipa faraja katika stori yangu kuwa imezaa matunda.

Nilifanikiwa kuwahoji Ofisa mipango,Katibu wa Afya na Ofisa habari wa Halmashauri kuhusu mikakati ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.

Target audience

Who did you hope to reach? Did you succeed in reaching this audience? What evidence do you have to that effect?

Nilipanga kukutana na wananchi,Viongozi wa Vijiji na Kata wakiwemo wauguzi na waganga kutoka katika Vijiji vyote vitano,wenyeviti wa Vijiji na watendaji wa Vijiji,wanakamati za huduma ya Afya za Vijiji,Diwani wa Kata na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.

Nimefanikiwa kuonana na baadhi ya wananchi,baadhi ya wauguzi,baadhi ya waganga,baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Afya,Diwani wa Kata,Katibu wa Afya wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya,Msemaji wa Halmashauri,Ofisa mipango wa Halmashauri na Mganga Mkuu wa Hospitali Teule ya Wilaya.

Nimefanikiwa kupiga baadhi ya picha za mnato za baadhi ya wananchi,Wauguzi na waganga katika zahanati katika baadhi ya vijiji,watendaji wa baadhi ya Vijiji,nimepiga pia picha za video za baadhi ya wananchi,baadhi ya wauguzi na waganga na baadhi ya Viongozi wa vijiji,pamoja na baadhi ya sauti nilizorekodi kwa wauguzi,wananchi,waganga,watendaji wa vijiji na Diwani.

Aidha ushahidi mkubwa unaweza kuupata katika mitandao ya kijamii,youtube na blog yangu kwa mfano face book/thompsonmpanji,mpanjimwanamai.blogspot.com,twitter/thompson mpanji na youtube/kmwamfum kapembamoto ikiwemo na makala iliyopo katika gazeti la Homa ya Jiji nililoliambatanisha katika fomu hii

How did you go about researching and writing the story?

How did you gather the data, how many sources, female and male did you consult? Why did you choose these sources and how were their voices important?

Nimetefanikiwa kupata baadhi ya takwimu katika Ofisi za Vijiji ikiwemo na kutembelea vijiji na kukutana na wahusika. Nimekutana na wanawake zaidi ya 10 na wanaume watatu kutokana na umuhimu wa wanawake ambao ndiyo walengwa katika huduma za afya ya uzazi.

Feedback

What impact did it have? What evidence do you have to illustrate impact?

Nimeandika habari hizo katika katika gazeti la Homa ya Jiji kama ambavyo nimeambatanisha katika fomu hii. Lakini pia katika kuhakikisha habari hii inawafikia walengwa ambao ni serikali na wadau mbalimbali wa huduma ya afya niliamua kusambaza katika mitandao ya kijamii kama katika mitandao ya kijamii mathalani kundi la whatsapp la ukatili wa jinsia,you tube mwamfumu kapembamoto,face book ya thompson mpanji na blog yangu ya www.mpanjimwanamai.blogspot.com,mwanawampanji.blog.

Aidha licha ya kuwatumia waandishi wenzangu wa habari kama gazeti la Mwananchi lakini pia ninaendela kuandika habari hizo katika maeneo yote na kushirikiana na waandishi wenzangu kwani kwa kuwashirikisha tutakuwa na sauti ya pamoja kwa kupiga kelele za pamoja na hivyo wahusika kusikia na kuweza kufuatilia.

Mafanikio yameanza kuonekana kutokana na Viongozi wa Halmashauri kwenda kutoa semina kwa wauguzi na waganga na pia wameahidi kutatua kero nyingine huku wakielezea kuwepo kwa mikakati kujenga kituo cha Afya.

MAFANIKIO

Tayari suala la ushuru kwa wakulima limeshughulikiwa baada ya wiki mbili tangu kufuatilia na kuandika habari hizo na sasa wakulima wanatozwa ushuru wa bidhaa walizoleta kama tenga/kikapu cha nyanya kwa sh.200 badala ya zamani ambapo tenga moja ambalo linadaiwa kuwa na plastiki ama debe tatu lilikuwa linatozwa sh.600.

Pia wataalamu wa halmashauri ya Wilaya ya Mbeya akiwemo na Ofisa mipango walitembhelea Kata nzima ya Igale kutoa elimu kwa wauguzi na madaktari kutoa elimu ya kuzingatia maadili mema ya uuguzi na udaktari baada ya kuandika habari

kuhusu kero walizokuwa wanakumbana nazo wagonjwana hasa akina mama wajawazito na watoto. Ufuatiliaji wa uwajibikaji unaendelea na ninatarajia kuandika habari zaidi ikiwemo na matokeo yake hadi mei,25,2016

Follow up

How would you conduct a follow up to your story and why?

Ninafanya ufuatiliaji wa habari yangu kupitia mawasiliano na wananchi waliopo katika Vijiji nilivyotembelea,wananipa taarifa ya kila kinachoendelea.

Lakini pia watendaji wa Vijiji nilishajenga mahusiano nao mazuri baadhi yao na wamekuwa wakinipa mrejesho wa kila kinaendela katika Vijiji vyao. Alikadhalika Halmashauri ya wilaya ya Mbeya kupitia Ofisa wao habari tayari tumeshajenga mahusiano mazuri na kila wanachokwenda kukifanya katika Kata ya Igale ananieleza na pale inapobidi kunishirikisha kwenda ninafanya hivyo bila kujali posho zao ambazo wamekuwa wakinieleza kuwa bajeti yao ni ndogo na hivyo inawatosha wao,hivyo ninalazimika kujigharamia chakula hadi tumapomaliza shughuli na kurudi majumbani.

Lakini pia ninapopata nafasi na kuwa na uwezo wa fedha za usafiri nimekuwa nikienda kutembelea zahanati na kuzungumza na baadhi ya wananchi kuhusu maendeleo na kero zilizopo endapo zimepungua ama kumalizika kabisa.

Nimekuwa nikifika katika baadhi ya zahanati mathalani Izumbwe na Shongo kutokana na ukaribu uliopo na kuulizia endapo kuna mikakak ya matumaini ya hivi karibuni ya kufikisha umeme ama kununua umeme unaotumia nguvu ya jua kwa ajili ya kutatua tatizo la akina mama wajawazito kuzalishwa kwa kutumia tochi za simu.

Kwa ujumla nimeweka utaratibu wa kufuatilia kujuwa endapo kuna mabadiliko yeyote ya kupungua ama kunmalizika kero kwa sababu ni jukumu langu kama Mwandishi wa habari kufanya ufuatiliaji wa habari niliyoiandika. Kwa sababu nimeandika habari ili ifanyiwe kazi ili kero zinazolalamikiwa zimalizike,nami ndiyo wajibu wangu kama

Mwandishi wa habari kupiga kelele za msingi,kuwa sehemu ya watu,kundi ama jamii ya wasiosikika ili mimi niwe kisemeo chao ama mdomo wao wa kufikisha ujumbe. Kwa hiyo sipaswi kulipua kazi bali ninatakiwa kufanyakazi kwa umakini bila mimi kuathirika wala wananchi waliotoa sauti kuathirika ili lengo la kuwasaidia watanzania wanyonge liweze kufikia kwa kupitia kalamu yangu. Nitapata faraja sana kuona kundi la watu ama jamii fulani iliyokuwa ikiteseka inapata unafuu,inapata huduma wanazostahili bila kunyanyaswa na hasa wanawake ambao walio na majukumu makubwa.

Click here