Women find new ways of breaking trust in the marriage_ Clouds TV_ August 2016


Date: August 24, 2016
  • SHARE:

Name of the story: Women find new ways of breaking trust in the marriage

Name of the media house: Clouds TV

Country: Tanzania

Synopsis

Brief description of the item of work you submitted and motivation of why it is a good example of gender awareness and sensitivity in advancing gender equality Post-2015.

WANAWAKE WAGUNDUA MBINU MPYA YA KUVUNJA UAMINIFU KATIKA NDOA BAADA YA KUFANYIWA UKATILI NA WAUME ZAO SUALA la unyanyasaji na ukatili wa kijinsia katika jamii ni jambo la kuendelea kuongeza nguvu katika kulipigia kelele kila kona ili familia zetu za kitanzania ziweze kujenga utamaduni na hulka ya kuamini kuwa binadamu wote ni sawa na wanastahili kupata haki zao msingi kama walivyo binadamu wengine.

Katika kuthibitisha hilo serikali imeweka wataalamu wa masuala ya maendeleo ya jamii na Idara ya ustawi wa jamii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama Tamwa,TGNP Mtandao na wengineo kuyashughulikia masuala ya haki sawa na haki za binadamu pia.

Zao la Kahawa katika halmashauri ya Wilaya ya Mbeya,ni zao kuu la biashara ambalo wananchi wake wanalitegemea sana kwa kuinua hali zao za uchumi na kuongeza mapato ya ushuru katika Halmashauri hiyo lakini bado kuna changamoto kubwa ambayo serikali na wadau wanapaswa kuongeza nguvu ya kutoa elimu ili kuwepo na usawa katika mgao kati ya mwanamke na mwanaume.

Clouds Tv imezungumza na baadhi ya wakulima wa Kijiji cha Izumbwe,Kata ya Igale,Elizabeth Mbwiga Jane Bryton ambao wanashauri kuwepo na semina kwa wanaume ili wajengewe uelewa kuwa mwanamke anayo haki sawa kama mwanaume ama kama binadamu mwingine.

Na katika hali ya kushangaza wanawake hao wamesema kuwa wamebuni mbinu nyingine ya kuiba sehemu ya kahawa wanapokwenda kuosha mtoni na kuiuza kwa kificho ili wajipatie fedha kwani waume zao wamekuwa hawawapatii fedha za matumizi.

kwa upande wake Sista Anthony ameelezea sababu ya kuanza kuvunja uaminifu kwa waume zao na kuiba kahawa huku Mratibu wa zao la Kahawa,halmashauri ya wilaya ya Mbeya,lupakisyo Masuba akithibitisha kuwepo kwa tatizo hilo na jitihada wanazozifanya.

Background

Why did you produce the story? What problem or context is it responding to?

Habari hii niliipata katika Kata ya Igale ambako kuna Vijiji vitano vya Shongo,Horongo,Igale,Itaga na Izumbwe,Nilifanikiwa kufika huko baada ya kubahatika kuhudhuria semina ya mrejesho ya TGNP kuhusu utafiti waliokwenda kuufanya katika nyanja za elimu,kilimo,Afya na maji.

Semina hiyo iliwashirikisha baadhi ya wananchi wa Vijiji vya Kata ya Igale na wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya akiwemo na Mkurugenzi. Mengi yalizungumzwa lakini nami nilivutiwa sana katika kujuwa masuala ya haki na usawa kwa wanawake katika na baada ya kufika katika Kata hiyo nikabahatika kuzungumza na baadhi ya wanakijiji wanawake na kuelezea changamoto wanazokabiliana nazo na mbinu mpya waliyoibuni ya kujipatia kipato pasipo mwanaume kugundua.

Key objectives

What did you hope to achieve with this coverage?

Lengo kubwa la kufuatilia na kuiandika hii habari ni kutaka wanaume wajuwe kuwa dhana potofu waliyonayo kuhusu mfumo dume katika sekta ya kilimo hauna tija na zaidi utaendela kurudisha nyuma maendeleo.

Kwa sababu mwanamke naye atashtuka na kuiba sehemu ya mazao na kujiuzia kwa kificho na kuendelea kujijenga kwa siri bila mume wake kujuwa na mwisho wake ni umaskini katika familia. Taarifa za uhakika ni kuwa mwanaume anapoenda kuuza mazao anazifuja ama kuzitumia fedha kwa hanasa kwa kunywa pombe na kuongeza wanawake,badala ya kutumika fedha kwa ajili ya maendeleo ya nyumbani. watoto hawaendelezwi na mwishowe ni umaskini ndani ya nyumba

Targets audience

Who did you hope to reach? Did you succeed in reaching this audience? What evidence do you have to that effect?

Clouds Tv inatazamwa Tanzania Bara na visiwani na kupitia website inaangaliwa karibu dunia nzima. Kwa hiyo ujumbe utakuwa umefika kwa wadau mbalimbali mathalani mashirika yanayojihusisha na masuala ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia na hivyo kuelekeza nguvu zao kuwakomboa wanawake kuondokana na huo mfumo dume.

Wanaume nao watasikia na hivyo kujibadili kwa kuondokana na dhana hiyo ya zamani iliyopitwa na wakati. Aidha kupitia maoni ya watazamaji baada ya kurushwa habari hii katika Tv ni mojawapo ya viashiria kuwa ujumbe umefika,lakini pia kupigiwa simu na ndugu,jamaa na marafiki waliotazama habari hiyo ni ujumbe pia umefika. Ushahidi wangu utakuwa katika chumba cha habari Clouds Media group.

How did you go about producing the programme?

How did you gather the data, how many sources, female and male did you consult? Why did you choose these sources and how were their voices important?

takwimu na wahusika niliyowahoji niliwapata moja kwa moja kutoka katika Vijiji vya Kata ya Igale

Feedback

What impact did it have? What evidence do you have to illustrate impact?

Mfano wa mrejesho kwangu binafsi bado sijaupata zaidi ya nambari za simu za ndugu,jama na marafiki walionipigia kwa mfano,0752 142610,0753804343 nk

Follow up

How would you conduct a follow up to your story and why?

Habari nitaendelea kuifuatilia kupitia mawasiliano ya simu kwa wananchi lakini na kwa kufika kutembelea na kuwahoji wanawake niliowahoji awali kujuwa maendeleo ya hali hiyo na hasa baada ya msimu wa mauzo kupita.

Lakini pia nitapata nafasi ya kuwahoji kujuwa mtazamo wao endapo hali itazidi nini kifanyike ili kuwaleta pamoja na waume zao na kuondoa dhana hiyo ya mfumo dume ya kutomjali mwanamke.

Mwanamke kuonekana kama chombo cha kukifanyisha kazi na kukaa nyumbani,mwanamke hapaswi kushika hela. Pia nitawasiliana na maofisa maendeleo na mtaalamu wa zao la kahawa kutoka Halmashauri kujuwa kinachoendelea na jitihada wanazoziweka katika kuhakikisha wanamkomboa mwanamke. Jitihada nyingine nitawatumia TGNP kujuwa mikakati yao baada ya kuibua masuala hayo. na mwisho nitawasiliana na wananchi waliofanya utafiti na TGNP ambao nao nilichukuwa nambari zao za simu kwa ajili ya kupata mrejesho